Mgen anapokuja nyumbani kwako utamkaribisha kwa glas ya juisi ,maji au chakula.kama ataendelea kuwepo kwa muda mrefu atampatia kitanda apimzike.Kama mgeni ni mwanamke atalala na watoto wakike.Kama ni Mwanaume atalala peke yake au na wanaumewenzake inapobidi.
Lakini katikamakabilaya Ovahimba na Ovazemba ya Namibia hali
ni tofauti kwani mgeni mwanaume anapofika,hukarimiwa kwa kupewa mke wa mwenye
nyumba afanye nae mapenzi.
Mtindo huu umekuwepo vizazi hadi vizazi ,lakini watunga
sheria sasa wanazungumzia uwezekano wa kitendo hicho kuingizwa katika sheria za
nchi hiyo,huku wengine wakipinga na kusema kitendo hicho kimekuwa
kikiwadharirisha wanawake.
Kitendo hicho kinajulikana kama “Okujepisa omukazendu” ikiwa
na maana “kumkarimu mgeni kwa kumpa mkeo “ Wenyeji wanasema ni uungwana kwa
mwanamume kumzawadia rafiki mke wake afanye nae mapenzi.
Katika kabila hilo watu wasiopungu 86,0000,wanaamini kuwa mgeni mwanaume anapaswa kukaribishwa kwa kupewa zawadi kubwa ambayo hawezi kusahau pale atakapoondoka.
Hata hivyo,wanawake hawana nguvu ya kukataa pale mume
anapoamua ,hubadilishwa kwa kilamgeni anayefika nyumbani .
Pamoja naNamibia kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya
virusi vya Ukimwi, jamii hii imekuwa ikijitetea kuwa haina ugonjwa huo kwa kuwa
haiingiliani na jamii nyingine zilizoathirika.
Kambapira Mutumbo (40) anasema haoni tatizo kumkaribisha
mgeni kama akipewa amri na mume wake kwa kuwa anasaidia kudumisha mila na
desturi.
Makabila haya yanatetea pia kitendi hiki yakisema
kinadumisha urafikibaina yao,kutunza utamaduni na kudhibiti uzinzi.
Mtandao wa Independent ulimkariri Kazeongere Tjeundo,ambaye ni mbunge na naibu
rais wa chama cha upinzani cha Democtatic Turnhalle Alliance of Namibia,akisema
Ni utamaduni unaounganisha watu ,lazima uenziwe na kutambulika nchini.
“Ni hiyari yako kumkabidhi rafiki unayemtaka alale na mkeo
,kwa sababu siyo jambo la kulazimishana.”Ninapendekeza itungwe sheria ya
kuwalinda “anaongeza Tjeundo.
Anaongeza kwa mfumuko wamagonjwa usiwe sababu ya kudidimiza
mila na kwamba serikali iangalie namna ya kuweka utaratibu utakaofanya jamii
hiyo ifanye ngono salama.
Hata hivyo kauli hiyo imewakera wanaharakati wa jinsia ambao
wanadai ni kitendo cha ukiukwaji wa haki za binadamu kwa kuwa mwanamke huwa
hausishwi kwenye maamuzi.
Mwanaharakati Rosa Namieses anasema kitendo hicho ni sawa na
ubakaji napia kinamuweka mwanamke katika hatari ya kuambukizwa Ukimwi.
Wanawake piahuruhusiwa pia kuwapawaume zao wageni wanawake wanapofika nyumbani kwao ili wafanye nao mapenzi ,lakini wivu wa
wanaume hukwamisha.
Makabila haya yapo Kaskazini Magharibi mwa jimbo la Kunene karibu
karibu na mpaka wa Angola na nayamejitenga na jamii nyingine.
Kuhusu makabila haya
Makabila haya ni ya wafugaji wanaume hufanya kazi ya
kuchunga na kuchinja na wanawake hukamua maziwa na kutunza familia.
Mavazi yao ni sketi tu na wake kwa waume huwa na vifua wazi wakati
wote.
Jamii hii hujitofautisha kwa mtindo wa nywele.Walioolewa au
kuoa huwa na msuko wa aina moja hali kadhalika wengine husuka kutokana na
wadhifa.
Wasichana hukeketwa na wavulana hutairiwa kabwa ya kubalehe
ili kumwandaa na ndoa.Mwananchi.
No comments:
Post a Comment