Kim na Kanye West
Watu maarufu kadhaa wamekataa kuhudhuria harusi ya Kanye
West na Kim Kardashian inayotarajiwa kufugwa mwezi ujao.
Watu hao ni kama vile Robin Thicker,Jared Leto,Jonah
Hill,Anna Wintour ,Oprah Winfrey,Will Smith na mkewe Jada,Prince,Karl
Lagerfed,Barack na Michelle Obama,Beyonce na Jay Z.
Obama na mkewe Michelle
Oprah Winfrey
Jay z na Beyonce
Will smith na Jada
Aidha ndoa hiyo inayosubiriwa kwa ham kubwa sana imeonekana
kuwa na garama ambapo inadaiwa kuwa katika harusi hiyo kuna wageni 200 ambapo
kila mmoja amewekewa gharama ya dola za Marekani 125,000.
Gharama hizo zitahusisha vitu mbalimbali na kufanya gharama
nzima kuwa dola za Marekani milioni 25.
Kuna tetesi kuwa kadi
za mwaliko kwa kila mtu imegharimu dola 1000,kwa kuwa wawili hao wanataka
wageni wao wawe wenye kuvutia siku hiyo.
Kwamujibu wa jarida la Grazia UK styleCaster lilitaarifu
kuwa ili kufanikisha azma hiyo ya wageni wao kuwasili wakiwa wamependeza
wametoa zabuni kwa wabunifu wa mavazi maalumu kwa ajili ya kuandaa vitu
mbalimbali kwa wageni hao.
Kuna kinywaji cha dola 500 huku kukiwa na kingine cha dola 200 huku kukiwa tena na dola 250 kwa ajili ya kuhudumiwa vitu mbalimbali vya mahitaji ya mwili kama vile kukandwa mwili katika hotel itakayofanyikia harusi hiyo
No comments:
Post a Comment