Pages

Wednesday, April 09, 2014

MATUMAINI YA KUPATIKANA MH370 YAKOLEA

                                              Operesheni ya kuitafuta MH370 inaendelea

Kiongozi wa operesheni ya kuitafuta ndege ya Malaysia ya MH370 iliyotoweka mwezi mmoja uliopita, Angus Houston wa Australia, amesema kuwa ametambua mawimbi ya sauti inayoaminika kutoka kwa kinasa sauti cha ndege hiyo maarufu kama 'black box' ya ndege hiyo.

Houston alisema kuwa kifaa maalumu kinachokokotwa na meli moja ya kijeshi ya Australia, Ocean Shield, kilipata mawimbi kamili kwa muda wa kati ya dakika tano u nusu na saba.
Mawimbi sawa na hayo yaliopatikana mwishoni mwa wiki na hii ina maana kuwa wataweza kulenga eneo ambalo inaaminika zaidi kuwa ndege hiyo ilianguka na kwa hivyo kuimarisha utafutaji wake.BBC

No comments:

Post a Comment