Uvumi umezuka kuhusu kuenea Ebola
Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa kuzuka
kwa Homa ya Ebola Magharibi mwa Afrika ni mojawapo ya changamoto kubwa
zaidi ambazo limewahi kukabiliana nayo.
Shirika hilo limesema kuwa italichukua hadi
miezi minne kuthibiti ugonjwa huo. Wakati huohuo shirika la kutoa
misaada ya matibabu ya bure, Medicins Sans Frontieres, limesema kuwa
linaendelea kufanya mashauriano na viongozi wa kijamii katika Wilaya
moja Kusini mwa Guinea, ambalo lilisimamisha shughuli zake baada ya
vituo vyake kadhaa kushambuliwa na wakaazi wa eneo hilo.
Msemaji wa shirika hilo katika mji mkuu wa Guinea wa Conakry - Sam Taylor - amesema inaeleweka kwamba watu wana uoga mkubwa.
"Sio taharuki, kimsingi huu ni uoga. Na
tunaelewa hilo. Ni ugonjwa wa kugovya na pia ni mpya nchini
Guinea, na
kuna uvumi unaosambaa na pia kuna habari za kuotosha zinazoenea; na
tunachohitaji kuona kwa wingi sasa ni watu kwenda kwa jamii mbalimbali
kueleza ugonjwa huu, jinsi unavyoenea, na jinsi usivyoenea," alisema
Bwana Taylor.
Ugonjwa huo umewaua watu 111 katika nchi za Guinea na Liberia tangu uchipuke mwezi uliopita.BBC
No comments:
Post a Comment