Pages

Thursday, April 10, 2014

UCHAGUZI INDIA WAINGIA HATUA MUHIMU

                                                   Uchaguzi India waingia hatua muhimu 

Leo ni siku muhimu zaidi katika uchaguzi mkuu nchini India-taifa ambalo ni demokrasia kubwa zaidi duniani. Uchaguzi wa ubunge unafanyika hivi leo katika majimbo mhimu, ikiwemo mji mkuu New Delhi.

Watu milioni mia nane na kumi na nne wana kibali cha kushiriki katika uchaguzi huo ambao unafanyika kwa kipindi cha wiki tano kutokana na sababu za kiusalama na miundo mbini.
Hadi kufikia sasa maeneo muhimu yaliyolengwa na vyama kinzani vya Congress na BJP yamekamilisha shughuli hizo.

Leo hii maeneo mengi yaliyokumbwa na ghasia yatafanya uamuzi wake, kukiwemo India Mashariki ambako waasi wa Kimao wametisha kuvuruga uchaguzi huo.
Maelfu ya maafisa wa usalama wa ziaza wametumwa kushika doria kutokana na umuhimu wa uchaguzi huo.

Katika uchaguzi huo maeneo muhimu yanayonganganiwa ni kama vile Kerala eneo la Kusini na maeneo mengine muhimu ya Jimbo la Kaskazini la Uttar Pradesh. Eneo ambalo pia linachunguzwa kwa makini ni ni lile linalozunguka Jiji la New Delhi, ambako kuna viti saba vya Bunge vinavyogombewa.

Lakini bado kuna awamu zingine mbili za upigaji kura baada ya ya leo na matokeo yenye yanatarajiwa katikati ya Mei.
Zaidi ya watu milioni 814 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huo.BBC

No comments:

Post a Comment