Chidi Benzi alimjeruhi vibaya msichana anayedaiwa kuwa
mpenziwake wa zamani,Mwanaisha Kiboye.Kwamujibu wa maelelzoaliyoipa Global TV
,Mwanaisha anasema alimkuta Chid Benz maeneno ya Buguruni akiwa na mpenzi wake
na kumsalimia hali iliyomchukiza rapper huyo aliyebinua meza waliyokuwa wamekaa
nakuanza kumpiga.
Hata hivyo Chidi Benzi aliyekamatwa na kupandishwa kizimbani
kwenye mahakama ya Ilala kwa kosa la kujeruhi na kukutwa na bangi,ametoka nje kwa
dhamana ya shilingi laki moja,kitendo ambacho kimewasikitisha ndugu wa
Mwanaisha wanaosema alimjeruhi mno kiasi cha kukaribia kumuua .
“Ukiangalia mgonjwa mwenyewe baada ya muda anapata fahamu
,anaweza akapoteza fahamu nusu saa.Kwa hiyo hapa tunafanya process za kufanya
CT-Scan ya kichwa na ambayo gharama yake ni laki 3 kwa private na laki mbili
kwa Serikali”alisema Oliver ambaye ni rafiki wa Mwanaisha.Bongo5
No comments:
Post a Comment