Pages

Tuesday, March 18, 2014

WANAMICHEZO WANAOPENDWA ZAIDI DUNIANI



1.NEYMAR,BRAZIL-SOKA

Nyota huyu anaitwa pere wa baadaye,Akiwana umri wa miaka 22 Neymar raia wa Brazil anayechezea klabu ya Barcelona ya Hispania anapendwa na watu wengi  sehemu mbalimali hapa duniani kwa sababu ya kipaji cha kutangaza soka alichonacho.Tayari kampuni  za Panasonic,Volkswagen,Red Bull,Unilever na Nike yamemshika nyota huyu katika matangazo.

2.RORY MCLLROY,IRELAND YA KASKAZINI-GOFU

Rory Mcllory ni kijana mwenye umri wa miaka 24 na tayari ameshinda mashindano ya wazi ya gofu ya marekani .pia ameshinda taji linguine la Marekani la PGA katika michezo wa gofu.Mcllroy tayari ana mikataba na kampuni kama Nike,Jumeirah Estates,Oakley,Audemars piguet na Santander.


3.LIONEL MESSI,ARGENTINA-SOKA

Gazeti la nchini la nchini Marekeni liliwahi kumuita ‘King Leo’ Messi ni mchezaji mwenye ujuzi nakipaji  cha hali ya juu anayechezea klabu ya soka Barcelona ya Hispania.Ameshinda mara  tatu tuzo ya mchezaji bora Dunia.Pia akiwa na klabu yake ya Barcelona ametwaa mataji mengi .Kampuni nyingi tayari zimemkumbatia nyota huyuambazo ni Pepsi,EA Sports,Audemars piguet,Dolce &Gabana na Herbalife.

4.USAIN BOLT,JAMAICA RIADHA.

Bolt anajulikana kwa umahiri wake wa kukimbia mita 100,200 na mbio za kupokezana vijiti kwani katika olimpiki na mashindano ya Dunia amekuwa akitwaa medali za dhahabu.Bolt ana mkataba mkubwana puma.

5.CRISTIANO RONALDO,URENO SOKA

Ronaldo anaeichezeea timu ya Real Madridhajaingusha timu yake kwani amekuwa akifunga mabao karibu kila mechi vi na hivi sasa anashikilia tuzo ya mchezaji bora waDunia.Ronaldo ana mikataba mikubwan makampuni za Nike na Castrol.

6.BLAKE GRIFFIN,MAREKENI-KIKAPU

Ni mchezaji kijana ambaye hana muda mrefu katika ligi kuu ya kikapu nchini marekani (NBA).Hata hivyo katika muda huo mfupi GRIFFINN aamekuwa ni nyota  nyota kwa kufunga stili ya ‘Dunk’Griffin ameiwezesha klabu yake LA Clippers kuheshimia kuheshimika.Tayari anamikataba kama Kia,AT  &T na subyway.

7.NOVAK DJOKOVIC,SERBIA-TENESI

Djokovic mchezaji wa tenesi anayependwa na watu wengi .Ametwaa mataji yote sita makubwa ya Grand Slam,pia anamikataba mikubwa  na kampuni za Adidas,Audemars-piguet na Mercedes Benz.

8.SABASTIAN VETTE,UJERUMANI-F1

Akiwa na miaka 26 ni dereva mdogo kutwaa ubingwa wa mashindano ya magari ya formula 1 (F1)na tayari ametwaa ubingwa huo mara nne mfululizo na mkataba na kampuni ya Red Bull.

9.TIM TEBOW ,USA-AMERICAN FOOTBAL

Alikuwa mchezaji mahiri wa timu ya Denver Broncos inayoshiriki katika mchezo unaofahamika sana kama American Football.Lakini timu hiyo ya Broncos ilionekana haimuamini sana hivyo akahamia klabu ya  New York Jets na kupata mafanikio makubwa na kupendwa na watu wengi.Tebow anamkataba na makampuni ya Nike na Jockey

10.YANI-TSENG,TAIWAN-GOFU

Kwa watu wanaofuatilia mchezo wa gofu wanampenda sana Yani Tseng,kwasababu msichana huyu akiwa na miaka 25 tu tayari ametwaa mataji  makubwa matano ya Grand Slam kwa upande wa wanawake na mara mbili amekuwa mchezaji bora wa mwaka.Tayari anamkataba na makampuni ya Acer na Taiwan mobile.




No comments:

Post a Comment