Ndugu wa abiria waliokuwa kwenye ndege ya Malaysia
Jamaa za abiria wa China waliokuwa kwenye ndege ya
Malaysia iliyopotea,wametisha kususia chakula ikiwa maafisa wa utawala
wa Malaysia watakosa kutoa taarifa kamili kuhusu ndege hiyo siku 11
zilizopita.
Jamaa hao wameelezea kukerwa mno baada ya mkutano na maafisa wa shirika la ndege hiyo mjini Beijing.
Maafisa wa Malaysia nao wanasema kuwa wanafanya kila wawezalo katika kuisaka ndege hiyo.
Ndege hiyo MH370 ilitoweka tarehe nane mwezi Machi ikiwa imewabeba watu 239.
Nchi 25 zinahusika na juhudi za kuisaka ndege hiyo huku China ikianza kuitafuta katika ardhi yake.
Watu 153 raia wa China walikuwa kwenye ndege hiyo iliyokuwa inatoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing.
Vyombo vya habari nchini China vimekuwa vikikosoa juhudi za Malaysia katika kuitafuta ndege hiyo.
Baadhi ya jamaa za wachina wanasema kuwa
wanaamnini serikali ya Malaysia imebana taarifa kuhusu ndege hiyo na
wanataka maelezo zaidi kuihusu.
Baada ya kukutana na maafisa wa shirika la ndege
siku ya Jumanne, familia za waliokuwa kwenye ndege hiyo walitishia
kususia chakula
"Tunachokitaka ni ukweli,'' alisema mwanamke mmoja.
Wakati huohuo, nchi jirani ya Malaysia, Thailand
imesema kuwa jeshi lake limetambua kile linachosema ni Data za mtambo
wa Rader ambazo huenda zilitoka kwenye ndege hiyo.
Inasema kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea
Magharibi baada ya kupoteza mwelekeo. Hii inathibitisha madai ya hapo
ya awali ya jeshi la Malaysia.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment