Urusi inaunga mkono mpango wa crimea kupiga
kura ya maoni kujiunga na Urusi.
Balozi wa Urusi ndani ya Umoja wa Mataifa ameuambia mkutano wa dharura wa Baraza la usalama kuwa Moscow haitaki vita na Ukraine.
Vitaly Churkin alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Waziri mkuu wa mpito wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk.
Hata hivyo ametetea juu ya haki ya Crimea kupiga kura ya maoni kuhusu kujiunga na Urusi au la.
Yatsenyuk ameliambia Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa
Moscow imekua ikikiuka Sheria na mikataba ya kimataifa, hata hivyo ana
matumaini kuwa watakuwa na nafasi ya kuupatia suluhu mzozo uliopo kwa
njia ya amani.
Kwingineko, mashariki mwa Ukraine mjini Donetsk, mtu mmoja ameuawa wakati wa vurugu za waandamanaji mahasimu, maofisa wameeleza.
Watu kadhaa pia wamejeruhiwa wakati mamia ya
waandamanaji wanaoiunga mkono Urusi walipopambana na waandamanaji
wanaoiunga mkono Kiev.
Machafuko haya yanaelezwa kuleta athari kubwa tangu kuanguka kwa Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych, tarehe 22 mwezi Februari.
Kumekuwa na hali ya mvutano mkubwa wa kidiplomasia wakati kura ya maoni ikitarajiwa kupigwa na Raia wa Crimea.Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment