Familia ya bilionea namba
mbili nchini Marekani, Warren Buffett imeunga mkono juhudi za kupambana na
ujangili nchini kwa kuchangia helikopta moja.
Familia ya Warren Buffett imeamua kutoa
msaada huo kupitia Mfuko wa Howard Buffett Foundation, baada ya kuridhishwa na
hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali.
**************************
Balozi wa Urusi ndani ya Umoja wa
Mataifa ameuambia mkutano wa dharura wa Baraza la usalama kuwa Moscow haitaki
vita na Ukraine.Vitaly Churkin alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Waziri
mkuu wa mpito wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk.
Hata hivyo ametetea juu ya haki ya
Crimea kupiga kura ya maoni kuhusu kujiunga na Urusi au la.
****************************
Aliyekuwa
waziri mkuu wa Libya, Ali Zeidan, amepuuzilia mbali kura ya kutokuwa na imani
naye iliyotangazwa na Bunge la taifa hilo mapema juma hili iliyopeleekea
kufutwa kwake.
*******************************
Mwendesha
mashtaka mkuu wa mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC, Fatou Bensouda amesema
huenda akakata rufaa hukumu iliyotolewa kwa mbabe wa zamani wa kivita nchini
Congo Germain Katanga.
No comments:
Post a Comment