Putin na Obama
Rais wa Urusi Vladmir Putin ametia saini ilani ya
katiba inayotambua jimbo la Crimea kama taifa huru. Hatua hiyo inajiri
muda mfupi baada ya marekani na Muungano wa Ulaya kutangaza vikwazo
dhidi ya maafisa wa serikali ya Urusi na wa Ukraine waliohusika na njama
ya Moscow kuiondoa Crimea katika Ukraine.
Rais Obama amesema kuwa anataka kuweka bayana
kwamba kutakuwa na adhabu kwa wale walioanzisha mikakati ya Crimea
kujitenga na Ukraine akiongeza kuwa vikwazo zaidi vitatolewa. Hata hivyo
amesisitiza kuwa bado kuna njia ya kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya
kidiplomasia.
Awali
bunge la Crimea lilitangaza rasmi kuwa jimbo hilo liko huru kutoka kwa
Ukraine na kutoa maombi ya kujiunga na mataifa yanayobuni muungano wa
Urusi. Balozi wa Marekani nchini Ukraine, Geoffrey Pyatt, ameiambia BBC
kwamba ilani iliyotiwa saini na rais Putin kutambua uhuru wa Crimea
haitabadili mtizamo wa Marekani kuhusu hali ilivyo.
" Kadri marekani inavyozingatia, hapatakuwa na
mabadiliko kuhusiana na makadirio yetu kuhusu hali, mtizamo wetu wa
Crimea kama sehemu ya Ukraine iliyo huru na mtizamo wetu kuhusu kwamba
kura ya maamuzi ya siku ya jumapili iliyofanyika baada ya uvamizi wa
kijeshi uliotekelezwa na Urusi ni kinyume na sheria kwa vyovyote,"
anasema.
Msemaji wa Ikulu ya White House Jay Carney, alipoulizwa na waandishi
wa habari ikiwa rais Putin atalengwa baadaye na vikwazo hivyo amesema
kuwa Marekani haitawasaza baadhi ya watu katika uwezekano wa kuwawekea
vikwazo.
"Uwezo wa kutoa vikwazo dhidi ya watu mbali
mbali upo. Tutatoa tathmini kuhusu hatua mwafaka wakati hali ikiendelea
kubadilika. Hatutawasaza baadhi ya watu. Kutakuwa na gharama kwa Urusi,
Gharama ya ziada itakayotolewa kwa Urusi, ikiwa Urusi hatabadili
mwelekeo hapa kuhusiana na jinsi inavyoshughulikia hali nchini Ukraine,"
anasema.
Miongoni mwa maafisa waliolengwa na vikwazo vya
Marekani na Muungano wa Ulaya ni maafisa wa ngazi ya juu katika utawala
wa jimbo la crimea, rais wa Ukraine aliyengolewa madarakani Viktor
Yanukovich, naibu waziri mkuu wa Urusi, wabunge wa Urusi na makamanda wa
jeshi.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment