Pages

Tuesday, March 18, 2014

SARATANI SIO UGONJWA WA KISASA


                                Ugunduzi huu ni muhimu katika kusaidia watafiti kubaini chanzo 
                                cha Saratani

Watafiti nchini Uingereza wamegundua kuwepo Saratani katika mifupa ya kijana mmoja aliyeishi nchini Misri miaka elfu tatu iliyopita.

Hii ni miaka elfu mbili kabla ya kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuthibitishwa.

Mtafiti Michaela Binder, aligundua kuwa mifupa hiyo, ilikuwa na mashimo, na kugundua kuwepo aina ya Saratani katika mifupa hiyo.

Ugunduzi huu unaonyesha kuwa Saratani sio ugonjwa wa kisasa tu na hivyo wanasayansi watapata kuchunguza ambavyo ugonjwa huu ulianza miaka zaidi ya elfu moja iliyopita. CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment