Pages

Tuesday, March 18, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI




Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu amesema kitendo cha Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kubadilisha kanuni kwa kutoa muda zaidi wa kuwasilishwa kwa rasimu ya katiba hakimfurahishi.

Lissu alisema kitendo kama hicho ndicho kilichomfanya yeye na mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kutaka kujiuzulu mara mbili kutokana na kupingana na wajumbe wenzao.
                                    
                                    ******************************
Rais wa Urusi Vladmir Putin ametia saini ilani ya katiba inayotambua jimbo la Crimea kama taifa huru. Hatua hiyo inajiri muda mfupi baada ya marekani na Muungano wa Ulaya kutangaza vikwazo dhidi ya maafisa wa serikali ya Urusi na wa Ukraine waliohusika na njama ya Moscow kuiondoa Crimea katika Ukraine.
                         
                       **********************
Watafiti nchini Uingereza wamegundua kuwepo Saratani katika mifupa ya kijana mmoja aliyeishi nchini Misri miaka elfu tatu iliyopita.
Hii ni miaka elfu mbili kabla ya kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuthibitishwa.

No comments:

Post a Comment