Pages

Tuesday, March 25, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI




Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule, wanakwenda shule bila kukosa hata kama hawana uwezo wa kumudu mahitaji maalum ya shule.Rais amesema hayo Wilayani Korogwe wakati akipokea taarifa ya Wilaya iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bw. Mrisho Gambo.

 


Mamlaka ya usalama wa safari za baharini nchini Australia imesema kuwa operesheni ya kuitafuta ndege ya shirika la Malaysia iliyotoweka imesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa na mawimbi makali baharini. Taarifa zinasema kuwa upepo mkali pamoja na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo ina maana kuwa ndege hazitoweza kupaa kwa usalama. Mawimbi makali yameilazimisha meli ya jeshi la wanamaji wa Australia kuondoka katika eneo ambalo mabaki yanayodhaniwa kuwa ya ndege hiyo yalionekana hapo jana Jumatatu.




Viongozi wa kundi la mataifa saba tajiri zaidi duniani, G-7, wanafanya mazungumzo kwa siku ya pili mfululizo hivi leo mjini Hague, Uholanzi ajenda kuu ikiwa ni hatua ya Urusi kunyakua jimbo la Crimea kutoka Urusi.

No comments:

Post a Comment