Viongozi wa kundi la mataifa saba tajiri zaidi
duniani, G-7, wanafanya mazungumzo kwa siku ya pili mfululizo hivi leo
mjini Hague, Uholanzi ajenda kuu ikiwa ni hatua ya Urusi kunyakua jimbo
la Crimea kutoka Urusi.
Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998, Moscow
imenyimwa kiti katika kongamano hilo. Mkutano wa dharura wa G-7
uikubaliana kufutilia mbali kundi la G-8, kundi la mataifa manane tajiri
zaidi duniani, ambalo linaishirikisha Urusi.
Viongozi wa mataifa ya kundi hilo wameonya kuwa vikwazo zaidi vitatolewa
iwapo Urusi itaingia maeneo ya mashariki au Kusini mwa Ukraine ikiwepo
kulenga sekta ya kawi nchini Urusi. Lakini Marekani kadhalika
imesisitiza kuwa fursa ya kusuluhisha mzozo huo wa njia ya kidiplomasia
ingalipo.BBC
No comments:
Post a Comment