Kanye West akiwa na mzazi mwenzie Kim.
Mbinu za mama mzazi wa mkali wa vipindi vya runinga Kim Kardashian Kris Jenner,zimezaa matunda baada ya mwanamuziki Kanye West,kukubali kuachiamali za mchumba wake hata baada ya kumuoa.
West alikubali kuandikishiana hati ya makubaliano kabla ya ndoa,na miongoni mwa mambo ambayo atakuwa akimfanyia mwanamama huyo ni pamoja na kumlipa Dola milioni moja kila mwaka katika kipindi chote cha ndoa yao.
Kanye pia atamuachia Kimnyumba yao mpya iliyopo Bel Air,Los Angeles,ambayo imeandikwa jina la mwanamama huyo,vilevile fedha zote zitakazopatikana kupitia Kim ikiwemo matangazo,kipindi cha 'Keeping with Kardashian' zitaendelea kuwa za Kim.
Awali mama wa Kim alimtaka mwanamuziki huyo kukaa mbali na shughuli za kifedha za binti yake Kim,kwa madai anaingilia maisha binafsi ya mwanaye badala ya mapenzi.
No comments:
Post a Comment