Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, Alhaji Zuberi
Mbyana, anadaiwa kushindwa kuchukua hatua kwa watendaji wawili wa Mtaa
wa Chamwenda, Kata ya Nyakato ambao walitoroka na fedha za wananchi.
Watendaji hao; Titus Stario aliyekuwa kaimu mtendaji wa mtaa huo kati
ya mwaka 2011 hadi 2013 na Dorcas Siwari aliyedumu katika wadhifa huo
kwa miezi miwili mwaka 2013 kisha kutoka na fedha za wananchi sh milioni
1.5.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Chamwenda, Lucy Kapumse na Mtendaji wa Kata ya
Nyakato, Masegenghe Mathias, walithibitisha tuhuma hizo na kwamba
walishamwandikia barua mkurugenzi wa manispaa ili wasakwe na kuchukulia
hatua, lakini hadi sasa bado hawajakamatwa.
No comments:
Post a Comment