Watu 18 wamefariki
dunia, wakiwemo polisi wanne na viongozi wote wa kijiji katika ajali mbaya
iliyotokea Kijiji cha Utaho, Kata ya Puma wilayani Ikungi, Mkoa wa Singida,
ikilihusisha basi lenye namba za usajili T 799 BET aina ya Nissan mali ya
Kampuni ya Sumry.Ajali hiyo ilitokea juzi usiku saa 2.45 katika barabara kuu ya
Singida- Dodoma umbali wa kilomita 15 kutoka Singida Mjini wakati basi hilo
likitokea mkoani Kigoma kwenda jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, Alhaji Zuberi Mbyana, anadaiwa kushindwa
kuchukua hatua kwa watendaji wawili wa Mtaa wa Chamwenda, Kata ya Nyakato ambao
walitoroka na fedha za wananchi.Watendaji hao; Titus Stario aliyekuwa kaimu
mtendaji wa mtaa huo kati ya mwaka 2011 hadi 2013 na Dorcas Siwari aliyedumu
katika wadhifa huo kwa miezi miwili mwaka 2013 kisha kutoka na fedha za
wananchi sh milioni 1.5.
Mwenyekiti wa
iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amedokeza kuwa kwa
tabia na mwenendo wao, watawala wamemsaliti Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.Jaji Warioba amekemea pia tabia ya watawala kumtumia Mwalimu
Nyerere kama hirizi wanapotaka kupitisha mambo yao, huku wakimsaliti kwa matendo
yao.
Maandamano
makubwa ya kwanza yanatarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Nigeria- Abuja
baadaye leo watu wakiitaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwanusuru wasichana
200 wa shule waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislam .
Mkutano
wa kumi na mbili wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaaanza rasmi hii
leo mjini Arusha nchini Tanzania.Miongoni mwa maswala muhimu yatakayojadiliwa
ombi la Sudan Kusini kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment