Pages

Wednesday, April 30, 2014

HII SHERIA NI KIBOKO....WEZI KUKATWA MIKONO WAZINZI KUPIGWA MAWE

Serikali ya Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za kiisilamu.
Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia wiki hii.


Adhabu zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga mawe hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya kushiriki Zinaa.

Sheria hii itatekelzwa katika awamu tatu katika kipindi cha miaka mitatu.
Umoja wa Mataifa tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo.

No comments:

Post a Comment