Mtuhumiwa wa mauaji Germain Katanga
Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC imempata na hatia
ya uhalifu wa kivita mbabe wa kivita kutoka Jamhuri ya kidemokrasi ya
Congo, Germain Katanga.
Hata hivyo Katanga hakukutwa na hatia katika shtaka la udhalilishaji wa kijinsia.
Alituhumiwa kuhusika na mauaji ya wanavijiji zaidi ya 200 mwaka 2003
katika jimbo la Ituri lenye utajiri wa dhahabu, kaskazini mashariki mwa
Congo.
Katanga ni mtu wa pili kupatikana na hatia ya
uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC tangu ianzishwe mjini The
Hague, Uholanzi mwaka 2002.
Katika shambulio hilo lililotokea mnamo Februari
24, 2003 watu 200 waliuawa katika kijiji cha Bogoro karibu na mpaka wa
Uganda,Katanga wakati huo akiwa Kamanda wa kundi la waasi la Patriotic
Resistance Force of Ituri (FRPI) lililotekeleza mauahi hayo.
Mwendesha mashtaka amesema nia yao kuu ilikuwa kuangamiza kijiji kizima.
Germain Katanga kwa jina la utani Simba alikanusha mashtaka hayo yote dhidi yake.CHANZO BBC
Ukanda wa Afrika ya kati
No comments:
Post a Comment