Pages

Sunday, March 09, 2014

NDEGE YAHOFIWA KUZAMA NA ABIRIA 239




Wakuu wa Vietnam wanasema michirizi miwili mikubwa ya mafuta imeonekana katika bahari nje ya mwambao wa kusini wa nchi hiyo, huku msako unaendelea kutafuta ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia iliyotoweka Jumamosi asubuhi.

Inasemekana michirizi hiyo miwili sambamba ina urefu wa kama kilomita 15 hadi 20.
Ndege na meli kutoka nchi kadha zimekuwa zikifanya msako katika eneo la bahari baina ya Vietnam na Malaysia.

Usiku ulipoingia ndege hiyo ya aina ya Boeing 777 ilikuwa bado haikuonekana - ndege ilipoteza mawasiliano na waongozi wa radar saa mbili baada ya kuanza safari.
Ilikuwa imebeba abiria na wafanyakazi wa ndege 239. Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment