Pages

Wednesday, March 26, 2014

MARY J BLIGE KUTUMBUIZA KWENYE HARUSI YA KIM NA KANYE


Ama kweli ya kweli ya kale dhahabu ukweli huo umekuja kudhihirika baada ya rapa Kanye West kumtaka mwanamziki mkongwe Mary J Blige kutumbuiza kwenye harusi yake.Kanye anatarajia kufunga ndoa mei 24 mwaka huu jijini Paris Ufaransa na miongoni mwa wanamziki watakaotumbuiza ni Mary j kwamatakwa maalumu ya Kanye.

"napenda muziki wa Mary J Blige na kila ninapokutana nae kwenye muziki ni lazima niimbe wimbo wake wa "Everything" hiyo ndiyo sababu ya kutaka aimbe kwenye harusi yangu"
Kanye alizidi kufika mbali zaidi na kufafanua kuwa havutiwi na kuimba tu bali aimbe kama ilivyokuwa kwenye tamasha lake la mwaka 1997.

Mtu wa karibu na rapa huyo aliuambia mtandao wa Hollwood life,Kanye amesema kila shairi lililo katika wimbo huo wa Everthing linaonyesha mapenzi yake kwa Kim.

                                                       Kim na Kanye

No comments:

Post a Comment