Kuna aina nyingi za panya. Kuna wanaoishi katika mazingira
ya binadamu na wengine huishi porini. Wote hawa wamewekwa kwenye kundi linalojulikana kitaalamu kama ‘Genus Rattus’. Hata ivyo kwenye kundi hili,
kuna tofauti kutegemeana na mazingira wanamoishi. Lakini pia maumbile yao
yanawafanya watofautiane.
Kuna panya warefu
zaidi ya wengine, wapo baadhi wana mikia mifupi. Kadhalika wanatofautiana
kwa rangi. Wapo wa kijivu, brown na weusi ambao ndiyo maarufu sana kwa vile
wengi huishi katika mazingira ya binadamu.
Dondoo za maisha ya panya
-Ni viumbe wanaoishi kwa ushirikiano, wanapenda kulala
sehemu moja na kufanya mambo kwa pamoja. lakini mara nyingi panya wenye umbo
kubwa ndiye huheshimika kutokana na nguvu alizonazo.Ndiye yeye anayeweza kupata
chakula kingi.
Panya wakiwa wamelala pamoja
-Panya hujali na kumsaidia mwenzao aliyeumia kwasababu
zozote ,na hii ni kutokana na maisha yao
ya kidungu.Panya ambaye hana marafiki hujiona mwenye shida kubwa na mara nyingi
hujificha peke yake.
-Panya ni kiumbe mwenye akili sana na ndiyo maana binadamu
mara kadhaa amekua akimtumia kwenye shughuli mbali mbali, iwe kijeshi au
kijamii. Ni viumbe wepesi kupokea mafunzo na kuelewa.ona hapa chini mfano wa panya aliyepewa mafunzo ya kupiga tarumbeta.
-Aidha,Panya anatajwa kama kiumbe mwenye kumbukumbu
kubwa.panya hawezi kusahau njia aliyopita kwa mara ya kwanza,ana uwezo wa
kumbukumbu kila kitu kwa kufuata njia bila kupotea hata kama ni kwenye msitu.
-Panya wana tabia ya usumbufu,lakini wao hawapendi usumbufu
na mara nyingi hawapendi kukabiliana na hatari na badala yake huenda popote
kujificha.
-Panya wanaweza kuishi mpaka miezi 18 ingawa wengi wao hufa
mapema kabla ya kufikisha miezi 12.
-Utafiti
unabainisha kuwa panya ni viumbe wasafi hasa wale wanaoishi mazingira ya
watu.Hutumia muda mwingi mchana kuandaa sehemu za kulala usiku.Mara nyingi
hupenda kutembea usiku kutafuta chakula kwenye makazi ya watu.
No comments:
Post a Comment