Kajala Masanja
Ni madai mazito kwamba nyota wa movie za kibongo Kajala Masanja amehongwa
gari na mtu anaedaiwa kuwa ni kigogo wa Ikulu.Hii ndiyo habari ya mjini kwa
sasa na Risasi jumamosi limeifukunyua.
Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zipo hadi kwenye mitandao
ya kijamii hasa Instagram,Kajala alinununliwa Gari hiyo aina ya Toyota Brevis
lenye rangu ya bluu iliyoiva wiki mbili zilizopita mara baada ya kutuoa Bongo
akitokea nchini China ambako alikwenda kwa mambo yake binafsi.
Taarifa zinavyodai
Wasambaza taarifa wallidai kigogo kigogo huyo wa Ikulu ni
Yule Clement ambaye aliwahi kuwa na
uhusiano wa kimapenzi na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu.
“mmeisikia hii?Kajala amenunuliwa gari na Kile
[Clement],lina thamani ya shilingi milioni kumi na moja,Wemaalie tu
nakwambia.We ukisema cha nini wenzio wanajiuliza watakipata lini?
“kwanza mnajua bifu la Wema na Kajala lilitokana na
Clement?Alipoachana na Wema akatua kwa msichana mmoja anaitwa Naima,lakini
lakini akaona bado akaenda hadi kwa
Kajala.Wema alipogindua ndo akamnunia nakuanza ushoga na Aunt
Ezekiel.msambaza habari za mjini mmoja
aliiambia Risasi.
Alhamis
Juzi saa 9:06 alasiri,Kajala akapigiwa simu ambapo alipokea
na mahojiano yakawahivi:
Risasi:Mambo Kajala? Kajala
:poa tu mambo?
Risasi:mambo poa, eti,namba ya gari lako Toyota Brevis ni
ngapi?
Kajala:Mh yaani hata mimi mwenyewe sizijui,sijazishika kabisa.
Risasi:Sasa kuna habari kwamba hilo
gari kwamba hilo gari umenunuliwa na Clement,Yule aliyekuwa na Wema zamani.Kuna
ukweli wowote?
Kajala:Mh hizo habari si za kweli .Wapo watu wanajiita Team
Wema ndiyo wameamua kunipakazia hivyo,wameandika hadi kwenye Instagram,lakini
siyo kweli kabisa.
“mimi nimenunua hili gari kwa mtu.Aliniuzia kwa shilingi
milioni kumi na moja ,Sijahongwa wala sijanunuliwa.Kuna watu wanataka
kunichafua tu.
Kuhusu ushoga wao
kufa
Awali Kajala hakutaka kulizungumzia hilo lakini alipobanwa
alidai hana tatizo na Wema na kwamba kwa sasa yuko bize kutengeneza Filamu
zake.
Wema akwepa simu
Kwa upande wake Wema alipopigiwa simu hakupokea lakini siku
za nyuma aliwahi kuanika kwamba haamini kama Kajala,anaweza kutembeana
Clement.Hapo ni wakati ule wapo mashoga.
No comments:
Post a Comment