Pages

Saturday, March 29, 2014

BINTI ATAPIKA MISUMARI NA CHUPA

                                                     Pesa na chupa alizotapika Rebeca
                                                               Hii ni misumari
                                                   Rebeca akiwa kanisani akitapika
                                         Rebeca akiwa hoi baada ya kutapika

Maajabu binti Rebeca Ankobea amewashangaza watu baada ya kutapika Sarafu za fedha,vipande vya chupa,nondo,misumari,pesa za noti na mayai.

Rebeca mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Accra,Ghana ambaye alitokewa na maajabu hayo hivi karibuni ambapo kabla ya tukio hilo,alitumwa na shangazi yake aitwaye Tina katika soko la kasoa hakurejea kwa takribani mwezi mmoja.

Baada ya mwezi kupita alirudi nyumbani akiwa hajielewi na kufanya matendo yanayoendana na ushirikina,majirani wote waliamini ni ushirikina.

Shangazi yake pia aliamini hivyo:
"Niliamini ni ushirikina alipofika alikuwa hajielewi na alikohoa sana,nilipomhoji alisema alitekwa Maeneo ya Kasoa na kufanyiwa mambo ya ajabu na mganga wakienyeji maarufu kama Sakawa.

Shangazi aliamua kumkimbiza katika Kanisa la Building Faith Ministry International (BFMI) na kufanyiwa maombi ndipo alipotapika vitu hivyo baadaye alitulia na kuwa katika hali ya kawaida.

No comments:

Post a Comment