Wasanii maarufu wa muziki wa bongo fleva na hiphop watashiriki katika Tamasha la mwisho la good time ya ukweli na coke-cola itakayofanyika Coco Beach Dar es salaam Jumapili hii.
Tangu mwezi uliopita Coke-Cola Tanzania imefanya matamasha matano ya muziki katika miji ya Dar es Salaam,Mwanza,Arusha,Mbeya na Moshi kwa lengo la kuburudisha na kutoa fursa kwa vijana kufurahi pamoja.
"Tumehamasika na Jinsi vijana walivyojitokeza kwa wingi katika matamasha yaliyotangulia,"Ni matumaini yetu kuwa vijana wengi zaidi watamiminika Coco Beach jumapili hii kuwaona Diamond,Joh makini,Vanessa Mdee na Madee.
No comments:
Post a Comment