Kundi la wanamgambo wa kiislamu la
Islamic state limetoa ukanda wa video unaoonyesha mateka Alan Henning
raia wa Uingereza akikatwa kichwa.
Henning mwenye umri wa miaka 47
ambaye ni dereva wa texi kutoka kaskazini mwa Uingereza alitekwa nyara
mwezi Disemba mwaka uliopita alipokuwa akilifanyia kazi shirika moja la
kutoa huduma za misaada kwa wakimbizi nchini Syria.
Kundi la
Islamic State ambalo limechukua udhibiti kwenye maeneo ya mpaka kati ya
Syria na Iraq tayari lishawaua waandishi wa habari raia wa Marekani
James Foley na Steven Sotlof pamoja na mfanyikazi wa kutoa huduma za
misaada kutoka Scotland David Haines.
Mapema babake John Cantlie
raia wa Uingereza ambaye anashikiliwa mateka na wanamgambo wa Islamic
State aliomba kuachiliwa kwa mwanawe.BBC
No comments:
Post a Comment