Pages

Sunday, September 14, 2014

MILIONEA ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUVAA SHATI LA SH MILION 270




Milionea Pankaj Parakh mfanyabiashara maarufu nchini india ambaye baada ya kufikilia ajipongeze vipi siku yake ya kuzaliwa aliamua kutumia kilo nne za dhahabu kutengeneza shatiatakalo vaa siku hiyo.


Sherehe hiyo ya kutimiza miaka 45 iliwashtua watu waliohudhuria baada ya kubaini kuwa shati hilo lilitumia dhahabu halisi yenye thamani ya zaidi y Sh270 milion za kitanzania.

Kutokana na thamani kubwa ya shati hilo,milionea huyo aliweka ulinzi mkali ili asije kugeuzwa mgodi.inakadiriwa kuwa watu 20 lilitumia saa 3200 kwa zaidi ya miezi miwili kutengeneza shati hilo.Milionea huyo aliongeza kwa kusema alikuwa akipenda sana dhahabu tangu akiwa na umri wa miaka mitano na ndo maana alifikiria kufanya kitu Fulani na dhahabu.

No comments:

Post a Comment