Mkazi wa Kisukuru jijini Dar es Salaam, Irene
Ibrahim anadaiwa kujinyonga hadi kufa, ikiwa saa chache kupita tangu aage
kuwa anasafiri kwenda Marekani.Kamishna wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es
Salaam, Suleiman Kova alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, mwili wa
marehemu ulikutwa kwenye shamba la Abdalah Mshindo jirani na eneo alilokuwa
anaishi.
Wizara ya Mambo ya Ndani imetoa ufafanuzi kuhusu
ajira zilizositishwa na kusema siyo zile zilizoandikwa na vyombo mbalimbali vya
habari jana.Jana vyombo vya habari viliandika kuwa ajira 70 za Idara ya
Uhamiaji kwa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi Uhamiaji zilisitishwa baada ya kuwapo
na madai ya upendeleo.
Wakazi wa Kijiji cha Masusu, Kata ya Gisambalang
wilayani Hanang’ katika Mkoa wa Manyara wamepatwa na mshtuko kutokana na tukio
lenye utata la kuuawa mtoto Omary Hamis mwenye umri wa mitatu, kisha mwili wake
kutundikwa juu ya mti.Inadaiwa kuwa Omary aliuawa na watoto wenzake wawili
ambao ni wakazi wa kijiji hicho kwa kumpiga kwa fimbo kisha kumnyonga na
baadaye kuutundika mwili wake juu ya mti.
Watu wawili, baba na mwanawe, wamekufa baada ya
gari walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea Ikwiriri
kuacha njia na kugonga kingo ya Mto Kihoi na kupinduka.Kamanda wa polisi wa
Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 5:00 usiku,
eneo la Kihoi Ikwiriri na aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni
Ramadhani Nassoro aliyekuwa dereva na mwanaye Abuu Ramadhani.
Nchi ya Liberia imefunga mipaka
yake iliyo mingi ya kuingia nchini humo ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi
mapya ya ugonjwa Ebola.Hata hivyo katika kuongeza jitihada Zaidi nchi hiyo
vituo vya uchunguzi vimewekwa katika baadhi ya mipaka ya kuingia nchini humo
vikiwemo viwanja vya ndege.
No comments:
Post a Comment