Katika hali ile ile ya mwendelezo wa kutumikia maelekezo na maslahi ya
CCM dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa chama hicho, Jeshi la Polisi usiku
huu limevamia nyumbani kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA,
Wilfred Lwakatare na kumkamata housegirl wake.
Kama hiyo haitoshi, jeshi hilo la polisi limewakamata wafanyakazi
wengine wawili (house boys) wa Lwakatare. Hadi muda mfupi uliopita
vijana hao wawili, walikuwa wako Kituo cha Polisi Mbezi huku msichana wa
kazi wakizunguka naye kwenye gari la patrol bila kumfikisha kituoni.
Jeshi hilo la polisi kupitia kituo hicho cha Mbezi lilikuwa linawatisha
kila mtu anayekwenda hapo kituoni kuulizia sababu za vijana hao
kukamatwa, lakini hatimaye mmoja wa watu walioko kituoni hapo ametonya
kuwa polisi wanasema mmoja wa vijana hao kesi yake iko Arusha!
Kijana anayetaka kubambikiwa kesi huko Arusha ni mwanagenzi kabisa
mjini. Hata ukimwambia aende Chalinze au Wami hawezi kupajua.
Hatimaye mbinu za CCM kupitia jeshi la polisi ya kutaka kukichafua
CHADEMA au viongozi wake kwa kutumia kes za kubambikia ugaidi imerejea
tena...Udaku
No comments:
Post a Comment