Walimu nchini Nigeria wanafanya
maandamano ya siku moja kushinikiza serikali kuharakisha juhudi zake za
kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara na kundi la wapiganaji wa
kiisilamu la Boko Haram zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
Maandanamo hayo pia ni ya kupinga mashambulizi ya Boko Haram dhidi ya walimu.
Kiongozi mmoja wa walimu hao aliambia BBC kwamba zaidi ya walimu miamoja sabini wameuawa mwaka huu.
Alituhumu maafisa wa serikali kwa kutoongeza juhudi za kuwalinda walimu na badala yake kujihusisha zaidi na siasa.
Wakati huohuo, Marekani imetuma vikosi vyake
nchini Chad , nchi ambayo inapakana na Nigeria kama sehemu za juhudi
zake kusaidia katika kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara.
No comments:
Post a Comment