Maafisa nchini Colombia bado wanajaribu kuwanusuru
takriban watu thelathini waliozikwa wakiwa hai na mamia ya tani ya tope
pamoja na mawe baada ya mgodi haramu wa dhahabu kuporomoka usiku wa
jumatano.
Miili mitatu imepatikana lakini maafisa wanasema
kuwa udongo uliolewa chepechepe katika eneo hilo umefanya juhudi za
uokoaji kuwa ngumu .
Waokoaji wanajaribu kufukua udongo ili kuwanusuru watu waliozikwa .
Takriban mashine saba za kufukua udongo zimekuwa
zikihusika katika shughuli ya uokozi katika mgodi huo ulioko kusini
magharibi mwa sehemu ya Cauca.
Kando kando mwa mgodi huo wapo mamia ya jamaa na
marafiki ya wachimba migodi waliofukiwa ambao wanafuatilia kwa karibu
shughuli za uokoaji.
Lakini mmoja wa wazima moto amesema kuwa hamna matumaini makubwa Huku matumaiani yakizidi kudidmia , Rais wa Colombia, Juan Manuel
Santos ameulaumu uchimbaji migodi haramu kwa kusababisha vifo hivyo .
Amesema serikali yake inapigana vita dhidi ya uovu huo.
Lakini mwandishi wa BBC ameongezea kuwa kuna migodi kadhaa katika maeneo fiche nchini humo.
Ijumaa wiki iliyopita, wachimba migodi wengine
wanne walipoteza maisha yao huku sitini na tano wengine wakiathirika na
gesi ya sumu katika sehemu ya Antioquia.BBC
No comments:
Post a Comment