Mwandishi wa
habari wa siku nyingi, Peter Temba amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela
baada ya kushindwa kumpeleka mahakamani mshtakiwa aliyemdhamini katika kesi ya
kutorosha twiga kwenda Uarabuni.
Mgogoro
wa uwekezaji katika Shirika la Usafirishaji Dar es Salama (Uda) umechukua sura
mpya baada ya Bunge kuamua Mkurugenzi wa Simon Group inayoendesha shirika hilo,
Robert Kisena ahojiwe na Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kutokana na
kuingilia kati madaraka hayo.
Shirika
la kutetea haki za binadamu Human rights watch limeishutumu serikali ya Somalia
kwa kuwanyima wafungwa haki za uakilishi wa wakili na kuwashitaki raia wa
kawaida chini ya mahakama za kijeshi.Shirika hilo limesema kuwa mamia ya raia
wanahukumiwa kwa sheria kali wasizoelewa.
Mwanamke
mmoja, wa miaka 25, aliyepotea miaka 10 iliyopita, amewaambia polisi kuwa
alilazimika kuolewa na aliyemteka nyara na kisha kupata mtoto naye.Mwanamke
huyo, kutoka Santa Ana, ambaye jina lake halikutajwa, aliwasiliana na polisi
baada ya kumpata dadake katika mtandao wa Facebook.
No comments:
Post a Comment