Pages

Wednesday, April 16, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI





Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mwigulu Nchemba, amesema Tanzania haiwezi kuingia kwenye muundo wa shirikisho la serikali tatu kwakuwa haina uwezo wa kuziendesha.Mwigulu, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akichangia sura ya kwanza na ya sita za rasimu ya katiba ambapo alisema kuwa kwa mwaka Serikali ya Zanzibar wanakusanya sh bilioni 200-300, lakini matumizi yao katika kipindi hicho si chini ya sh bilioni 600.
 

Siku moja baada ya serikali kuonyesha hati ya makubaliano ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamegawanyika juu ya uwepo wake.Wakizungumza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baadhi ya wajumbe wametilia shaka hati hizo kwa madai kuwa zitakuwa zimeghushiwa kwa lengo la kuwapumbaza Watanzania.

Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutoka meli moja iliyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini.Maafisa wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo wanatumia, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege za uokoaji kuwaokoa watu waliokuwa katika meli hiyo.

Polisi nchini Nigeria wanasema kuwa shule ya mabweni ya wasichana imeshambuliwa katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo huku wasichana wakitekwa nyara.Wazazi wanasema kuwa zaidi ya wasichana miambili wametekwa nyara na washambuliaji hao.

No comments:

Post a Comment