JESHI la Polisi mkoani Simiyu
linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Songambele wilayani Maswa mkoani
hapa, kwa tuhuma za kutaka kumuua mtoto wake kwa kumtupa na kumtelekeza
nje ya nyumba ili aliwe na fisi. Kamanda wa polisi mkoani Simiyu,
Charles Mkumbo alisema ofisini kwake mjini hapa jana kuwa tukio hilo
lilitokea juzi majira ya saa nane za usiku wakati mtuhumiwa Baya Seni
(30) akiwa amelala na familia yake kijijini hapo, ndipo alipokurupuka
ndani akampiga mtoto wake Amos Baya (3) na kisha kumtupa na kumtelekeza
nje ya nyumba.
Alisema, Seni katika maelezo yake kituo cha polisi
alisema alifikia uamuzi huo kwa kuwa hakuona thamani ya mtoto wa kiume
kwenye familia yake kwani uzoefu umeonesha kuwa watoto wa kiume wakikua
hudai kupata mirathi kutoka kwa wazazi wao .
Alisema kinyume chake
watoto wa jinsia ya kike wakikua watamuongezea utajiri wa mifugo
atakapolipwa mahari ili waolewe na baada ya kuolewa hawawi mzigo tena
kwenye familia yake bali mzigo huo huhamia kwenye familia atakayoolewa.
Mtoto huyo aliokolewa na majirani baada ya kusikia kilio.
Mama wa mtoto
huyo Elizabeth Paulo alisema, mume wake alikuwa akimtesa sana mtoto wake
akimbagua kwa vile yeye ni wa jinsia ya kiume na kwamba hana faida
kwake.UDAKU
No comments:
Post a Comment