Mkazi wa Pasiansi wilaya ya Ilemela,Rose Mapunda (42)amefikishwa mahakani wilaya ya Nyamagana kwa tuhuma za kumchanja mwanaye mwili mzima kwa kutumia wembe.Wakili wa serikali Juma Sarige alidai machi 10 maeneo ya Pasiansi Wilaya ya Ilemela,mshitakiwa alimchinja mwanae Peter Fabian (12)kwa kutumi wembe .Sababu ya adhabu hiyo ni tabia ya kuwamalizia wenzie chakula na ukorofi.
Serikali ya Tanzania imefutilia mbali usajili wa shirika moja lisilokuwa la kiserikali kwa sababu ya kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja katika jamii.Shirika hilo kwa jina Sisi Kwa Sisi lilisajiliwa baada ya kudai kuwa malengo yake yalikuwa ni kusaidia jamii.Tanzania imesema imechukua hatua ya kufutilia mbali usajili wa shirika hilo kwa kukiuka sheria za nchi na kwenda kinyume na malengo ya usajili wake.
Leo ni siku muhimu zaidi katika uchaguzi mkuu nchini
India-taifa ambalo ni demokrasia kubwa zaidi duniani. Uchaguzi wa ubunge
unafanyika hivi leo katika majimbo mhimu, ikiwemo mji mkuu New Delhi.Watu
milioni mia nane na kumi na nne wana kibali cha kushiriki katika uchaguzi huo
ambao unafanyika kwa kipindi cha wiki tano kutokana na sababu za kiusalama na
miundo mbini.
No comments:
Post a Comment