Makamo wa waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Iran
amesema nchi yake haifikirii kumteua mtu mwengine kuiwakilisha nchi
katika Umoja wa Mataifa.
Taarifa iliyotolewa na Abbas Araqchi imesema
Iran itatumia sheria kupinga uamuzi wa Marekani wa kumkatalia visa Hamid
Abutalebi kuingia Marekani, ili kuwa mwakilishi mpya wa Iran katika
Umoja wa Mataifa mjini New York.
Bwana Abutalebi amehusishwa na kundi lilovamia
ubalozi wa Marekani mjini Teheran mwaka wa 1979, na nchini Marekani
baadhi ya wanasiasa wamepinga vikali uteuzi wa mwanabalozi huyo.
Marekani haikuwahi kumkatalia visa mwakilishi katika Umoja wa Mataifa, wenye makao yake makuu mjini New York.BBC
No comments:
Post a Comment