Pages

Friday, March 21, 2014

WEMA NA KAJALA KIMENUKA


Kimenuka upyaaa! Wale mashostito wawili katika kiwanda cha filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja ambao walikuwa marafiki wa kufa na kuzikana, wanadaiwa kuvunja rasmi ushosti wao, Ijumaa limenyetishiwa.

Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki wa mastaa hao, hivi sasa hali ni tete huku sababu mbalimbali zikidaiwa kuwa chanzo cha yote.

WEMA KARUDI KWA SNURA?
Chanzo hicho kilidai kuwa kila mmoja kwa sasa amechukua hamsini zake huku Wema akidaiwa kurudi kwa shostito wake wa zamani, mamaa wa Majanga, Snura Mushi.

KISA CHA SALUNI
Mpashaji wetu huyo alizidi kudai kuwa chanzo kikubwa ni kuwa mashosti hao walikutana katika saluni moja maarufu iliyopo Kinondoni, Dar ambapo Kajala alikuwa akitokea kwenye ‘shutingi’ ya filamu yake.
Ilidaiwa kuwa Kajala alifika saluni hapo akiendesha baiskeli iliyosababisha akaloa jasho sehemu kubwa ya mwili wake.

Ilisemekana kwamba Wema alipomuona Kajala alitaka kumkumbatia lakini Kajala alimkwepa kwa sababu mwili wake ulikuwa na jasho jingi, jambo lililomfedhehesha Wema na kununa.
“Yaani baada ya Kajala kukwepa kukumbatiwa, Wema aliumia sana.
“Alichokifanya Wema, alimrushia Kajala maneno makali akimhoji kwa nini alimfanyia hivyo wakati hawana tatizo lolote kati yao,” kilidai chanzo hicho.

KISA CHA NYUMBANI
Hata hivyo, chanzo kingine kilicholonga na Ijumaa kilidai kwamba kuna siku Kei alikwenda nyumbani kwa Wema, Kijitonyama Dar kwa lengo la kumchukua waende location (sehemu ya kurekodia sinema).DIAMOND ANANYIMA FURSA?
Ikadaiwa kuwa Kajala alipofika nyumbani hapo aliambiwa ‘bimkubwa’ huyo amelala na Diamond na huwa hawaamshwi.

Chanzo hicho kilidai kwamba Kajala aliwasiliana na Wema kwa njia ya simu na akamwambia asubiri ambapo msanii huyo alisubiri kwa muda mrefu bila mafanikio hivyo hawakwenda kushuti siku hiyo.
Pia chanzo hicho kilitiririka kwamba ushosti wa Wema na Kajala ulianza kupepesuka muda mrefu lakini uzi wa mwisho umekuja kukatwa na Diamond mara baada ya kurudiana na Wema.

KIVIPI?
Chanzo hicho kilinyetisha madai kwamba eti Kajala hampendi Diamond kwani jamaa huyo amekuwa akitumia muda mwingi kuwa na Wema hivyo kubana fursa ya mashosti hao kujiachia.

“Unajua kabla Diamond hajarudiana na Wema, Kajala alikuwa anaweza kufika pale kwa Wema na kuingia hadi chumbani kwa shosti wake lakini sasa inashindikana kwa sababu anakuwepo Diamond,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:

“Ndiyo maana Kajala ameona kama mbwai, mbwai tu! Kila mtu afe kivyake.”

HUYU HAPA KAJALA
Kwa upande wake Kajala alipopatikana, awali hakutaka kulizungumzia suala hilo lakini alipobanwa alidai kuwa hana tatizo na Wema na kwamba sasa yuko bize kutengeneza filamu zake.

BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
Alipotafutwa Wema na kusimuliwa mkasa mzima alisema kwa kifupi: “Mimi niko sawa, hakuna kitu na muda si mrefu watu watatuona tena pamoja,” alisema Wema.

SI MARA YA KWANZA
Wema na Kajala wamekuwa mashosti wa muda tangu Wema alipomlipia mwenzake faini ya Shilingi Mil. 13 mahakamani na kumuepusha kwenda jela baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka saba.
Hata hivyo, si mara ya kwanza kutibuana kwani mwaka jana waligombana lakini baadaye wakapatana.UDAKU

No comments:

Post a Comment