Mwenyekiti wa tume yamabadiliko ya katiba,Jaji Joseph Warioba
leo anakabiliwa na kibarua kigumu pale
atakapowasilisha Rasimu ya katiba mbele ya bunge maalumu la katiba ambalo
wajumbe wake wamegawanyika kimsimamo.
Kwa hatua hiyo Jaji Warioba atakuwa anahitimisha safari ya
miezi 20 ya tume ya mabadiliko ya katiba iliyokusanya maoni ya
wananchi,kuyachakata na kutoa Rasimu hiyo itakayojadiliwa na Bunge hilo.
***********************
Umoja wa mataifa na Muungano wa Ulaya zimeelezea wasiwasi
kuhusu mvutano wa kisiasa unaozidi kutokota kati ya serikali na vyama vya
upinzani nchini Burundi.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amelaani hali ya kisiasa nchini humo,akisema kuwa serikali inakandamiza uhuru wa kisiasa, uhuru wa kuongea na watu kukutana.
************************
Wizara ya usafiri ya Malaysia inasema kuwa imeomba ushirikiano
wa nchi zote kwenye njia mbili ambapo ndege iliyopotea juma lilopita huenda
kuwa imepita.
Imeomba msaada wa data kutoka Satelite na Radar na msaada katika shughuli za msako.
Uchunguzi pia unafanywa kuhusu marubani wawili wa ndege hiyo na nyumba zao zimepekuliwa
No comments:
Post a Comment