Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali
imenuia kumaliza kabisa Ujangili nchini,ikiwa ni hatua ya kunusuru wanyama walio
hatarini kutoweka katika hifadhi za taifa.
*******************************
Mtu mmoja amefariki dunia jana na
wengine 18 kujeruhiwa vibaya na zaidi ya watu 80 kunusurika kufa baada ya basi
la kampuni ya Hood likitokea Arusha kuelekea Mbeya kupasuka tairi ya mbele na
kupinduka.
********************************
Mkuu wa jeshi la anga la
Malaysia, amekanusha madai kuwa ndege ya Malaysia iliyotoweka, ilionekana mara
ya mwisho Magharibi ya rasi ya nchi hiyo, eneo ambalo ni mbali zaidi na njia
iliyostahili kupita.
Generali Rodzali Daud, amesema kuwa hawawezi
kupuuza uwezekano huo, lakini amesema madai kuwa mawasiliano ya ndege hiyo
yalinaswa na mtambo wa radar katika eneo hilo sio kweli.
*********************************
Maafisa wawili wa Polisi Nchini
Afrika Kusini wametiwa mbaroni baada ya picha za video kuonyeshwa kwenye
mtandao wakimvua nguo na kisha kumchapa vibaya mtu mmoja kutoka Nigeria.
**************NA****************
Mwanafunzi mmoja ameuwawa
katika maandamano yaliyofanyika katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Maafa hayo yalitokea pale wanafunzi wa Chuo
kikuu cha Khartoum walipofanya maandamano.
Kundi la kutetea haki za binadamu Amnesty
International, limesema mwanafunzi huo alifariki kutokana na majeraha ya risasi
baada ya makundi ya kiusalama kuwatawanya wanafunzi hao kwa kuwashambulia kwa
risasi, na vitoa machozi.
Ni ghasia za kupinga machafuko yanayozidi
huko Darful.
No comments:
Post a Comment