Zaidi ya wanafunzi 71 wa shule
ya msingi na sekondari mkoa wa tabora wamepata mimba kipindi cha miezi 11 iliyopita.Mkuu wa mkoa Fatuma
Mwassa alisema wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,kuwa wanafunzi
hao walipata ujauzito kuanzia april mwaka jana hadi sasa.
Alieleza kuwa wanafunzi 21 wa
shule ya msingi walipewa ujauzito,huku wanafunzi 50 wa sekondari wakipewa ujauzito na kufanya
jumla ya wanafunzi 71.
**********************
Maafisa wa serikali nchini
Yemen wamesema kuwa zaidi ya wahamiaji arubaini wa Kiafrika wamezama baharini,
baada ya mashua walimokuwa wakisafiria kuzama, katika pwani ya kusini mwa nchi
hiyo.
Manuwari ya jeshi la Yemen ambalo lilikuwa
katika eneo hilo, imefanikiwa kuwaokoa wahamiaji wengine wapatao thelathini.
********************
Wakati
juhudi za kuisaka ndege iliyopotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Malasyia kuelekea
Uchina zikiendelea, ndege moja ya Vietnam imeripoti kuwa imeona kitu
kinachofanana na mlango wa ndege kwenye ufuo wa bahari ya Kusini mwa Uchina
kwenye mwambao wa taifa hilo.
********************
Rais wa
Marekani Barrack Obama, amemualika waziri mkuu wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk,
mjini Washington kwa mashauriano kuhusiana na mzozo unaokumba taifa lake.
No comments:
Post a Comment