Pages

Monday, March 17, 2014

SABABU ZA WANAWAKE KUPATA CHUNUSI




Kutokwa chunusi ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi sana,baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kutafuta dawa ya tatizo hilo wengi wamekuwa wakipata matokeo hasi,jambo linalosababisha wengi kukata tamaa.

Hata hivyo unaelewa 99%  ya tatizo la chunsi kwa mwanamke ni mwanamke mwenyewe?
ULAJI USIO MAKINI:Ulaji wa vyakula vya mafuta humuweka mlaji kwenye hatari ya kupata chunusi.

NGUO CHAFU:Kulala kwenye foronya chafu pia kunakuweka kwenye hatari ya kupata chinusi.

KUJISHIKA USONI MARA KWA MARA:Wanawake wengi hupenda kujishika usoni kwa viganjavyao bila kuwa na uhakika wa usafi wa mikono yao.

UMAKINI KATIKA KUOSHA NYWELE:Vipodozi vya nywele huambatana na mafuta hivyo muoshaji asipokuwa makini katika kuosha huweza kusababisha mabaki ya mafuta kuingia usoni hivyo kuiweka ngozi kwenye hatari ya kupata chunusi.

ELIMU YA UTUNZAJI NGOZI:Ngozi ya kilamwanamke inatakiwa kufanyiwa 'scrub' ili kuondoa seli zilizokufa na kuwekewa mvuke.Ikiwa haya hayakufanyika pia huwa ni mwanzo wakupata chunusi.

KULALA NA VIPODOZI:Hili ni tatizo sugu kwa wanawake wengi.wanawake wengu hulala navipodozi bila kujua wanaiweka ngozi katika hatari ya kupata chunusi.

No comments:

Post a Comment