Serikali imeanza juhudi za
kujinasua kwenye lawama kwamba haifanyi juhudi za kutosha kupambana na ujangili
kwa kuwaaalika waandishi wa habari wa kimataifa ili kujionea kazi inayofanyika.
Tayari mwaandishi wa habari
kutoka Uingereza aliyeandika habari katika gazeti la Daily Mail,Martin Fletcher
kuwa Tanzania haifanyi jitihada zozote kukabiliana na ujangili amewasili
nchini.
***********************
Zoezi la kutafuta ndege ya
abiria ya Malaysia limeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya
sintofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu wa watu waliopotea wakiwa
katika ndege hiyo.
Mamlaka nchini Malaysia zinasema wameongeza
mipaka ya eneo la utafutaji, mara mbili Zaidi, huku China ikiwa imepeleka
mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kutafuta ndege hiyo.
**********NA*************
Maafisa wa
Marekani wamesema kuwa Waziri wa mambo ya nje John Kerry, amekataa kukutana na
Rais wa Urusi, Vladmir Putin, mpaka pale Moscow itakaporidhia mapendekezo ya
Marekani kuhusu kumaliza mzozo nchini Ukraine.
No comments:
Post a Comment