Lambert Mende Waziri wa habari na msemaji wa serikali ya DRC Congo
Waandishi wa habari wa kigeni,
wanadiplomasia, wanaharakati na wasanii mbalimbali wametiwa mbaroni na
polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wakiwemo waandishi wa
habari wa BBC.
Wanaharakati hao, ambao ni vijana kutoka nchini
Burkina Faso, Senegal na Congo, walikuwa na mkutano na waandishi wa
habari kuhusu jukwaa jipya la kijamii.
Mwandishi wa BBC Maud
Jullien anaripoti kuwa wanaharakati kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo, Senegal na Burkina Faso walikuwa na mkutano na waandishi wa
habari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa unaohusu kuundwa kwa
jukwaa jipya la kijamii la vijana wa Congo.
Hapo ndipo walipokamatwa na kupelekwa makao ya usalama wa taifa.
Waandishi
wa BBC ni miongoni mwa waliokamatwa na wanasema wamewaona polisi
wakiwapiga baadhi ya wanaharakati kwa kutumia marungu.
Lambert
Mende ambaye ni msemaji wa serikali ya Congo amesema mkutano huo haukuwa
halali na kusema kuwa raia waliokamatwa kutoka Senegal na Burkina Faso
ni wachochezi hatari kwa usalama wa taifa la Congo.
Nchi ya
Burkina Faso na Senegal zote zilikuwa na vuguvugu dhidi ya marais wao
walipojaribu kubaki madarakani baada ya muda unaoruhusiwa kwa mujibu wa
katiba ya nchi zao kumalizika.
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo atakamilisha muhula wake wa mwisho ifikapo Januari, 2016.
Watu
zaidi ya arobaini wameuawa katika vurugu zilizosababishwa na muswada wa
uchaguzi ambao ungemuongezea muda wa kukaa madarakani.bert MendeCOngo
No comments:
Post a Comment