Pages

Friday, June 20, 2014

HABARI KWA UFUPI



Mwishoni mwa mwaka jana taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zilionyesha kuwa Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto walio na umri chini ya miaka mitano, vinavyotokana na ugonjwa wa malaria.


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inajipanga kuja na mfumo wa kompyuta utakaoratibu taarifa zote zinazopakiwa mtandaoni ili kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na watu wasio na maadili ya uandishi wa habari.

Marekani imeiwekea Uganda vikwazo kwa kupitisha sheria zinazopinga mapenzi ya jinsi moja katika taifa hilo la Mashariki ya Afrika.Afisa wa mahusiano anayesimamia maswala ya usalama katika ikulu ya whitehouse Caitlin Hayden anasema kupitia kwa barua kwa wanahabari kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la Uganda mwezi Februari inakiuka haki za binadamu.

Serikali ya Kenya inasema kuwa washukiwa watano wa mauaji ya watu 50 mjini Mpeketoni Pwani mwa Kenya wameuawa.Taarifa hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka katika wizara ya usalama kuhusu mauaji hayo yaliyofanyika Jumapili usiku na Jumatatu

Rais wa zamani wa Liberia, ameanzisha harakati za kisheria kupinga amri ya kutumikia kifungo chake cha jela nchini Uingereza. Taylor alifungwa jela kwa uhalifu dhidi ya binadamu na anakataa kutumikia kifungo hicho Uingereza akisema kuwa ananyimwa haki ya kufurahia maisha yake.

No comments:

Post a Comment