Pages

Thursday, May 01, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI



Ofisa  Mwandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini, Silvanus Mzeru, ameuawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha.Mauaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu  Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Mabweni saba ya wavulana wa Shule ya Sekondari Ivumwe, mkoani hapa, inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), yameteketea kwa moto na kuteketeza vifaa mbalimbali vya wanafunzi wa shule hiyo.Moto huo ulizuka jana majira kati  ya saa tatu na nne asubuhi wakati wanafunzi hao wakiwa madarasani kuendelea na masomo yao.

Katika kile kinachoweza kutafsiriwa kama ubabe wa madaraka na kutoelewana ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Katibu Mkuu, Maimuna Tarishi, amepindua maamuzi ya Waziri wake, Lazaro Nyalandu na kuwarejesha kazini vigogo wa Wanyamapori waliokuwa wameng’olewa na waziri huyo.

Maandamano na vurugu zimefanyika leo siku ya siku ya wafanyakazi duniani katika mji mkuu wa Uturuki wa Istanbul na maeneo mengine duniani.Maafisa wa polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi pamoja na maji baada ya waandamanaji kukaidi marufuku ya kuandamana katika bustani Taksim.

Rais wa Urusi, Vladmir Putin, ametoa wito kwa Ukraine iyaondoe majeshi yake katika maeneo ya Kusini Mashariki mwa taifa hilo na kuanza mazungumzo kama njia mojawapo ya kusuluhisha mgogoro unaoendelea nchini humo.Ofisi ya Rais imesema kuwa wito huo ulitolewa katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na kiongozi wa Ujerumani, Chansela Angela Markel.

No comments:

Post a Comment