Mwimbaji wa nyimbo za injili Amoni Mwakalukwa ni mzaliwa wa Mbeya wilaya ya Kyela,na ni
mtoto wa kumi na moja kuzaliwa kwenye familia ya watoto kumi na mbili.Baba yake
alikuwa mchungaji hivyo kumfanya akue katika mazingira mazuri sana ya kumjua
Mungu .
Amoni ambaye rasmi
kabisa alianza kuimba mwaka 2008 na alifanikiwa kutoa albamu yake ya kwanza
iliyoitwa “Injili ya msamaha” aliyofanya
na producer Chaina Praise Studio ambayo haikufanya vizuri sokoni.
Amesema mwaka huu
amejipanga viruri na hatimaye kuweza
kufanya albamu mpya ambayo inakwenda kwa jina la “Nitetee” akizungumza na blog ya Maisha yetu akasema “Hivi nimejipanga vyema
katika kufanya uzinduzi wa albamu yangu ya “Nitetee”utakao fanyika tarehe 8/06/2014.
Pia Amon amewashauri waimbaji wa nyimbo za injili kuendeleza
mazuri wanayoyaimba hata katika jamii akisema
“Waimbaji tujitahidi kuishi kama tunavyoimba siyo tuimbe kwa kutoa ujumbe mzuri
na tuishi kwa kutenda maovu.
No comments:
Post a Comment