Maandamano makubwa ya kwanza yanatarajiwa kufanyika katika mji
mkuu wa Nigeria- Abuja baadaye leo watu wakiitaka serikali kuchukua hatua zaidi
kuwanusuru wasichana 200 wa shule waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislam .
Wasichana hao walichukuliwa kutoka shule yao ya malazi iliyopo katika eneo
lisiloweza kufikiwa kwa urahisi kaskazini mashariki mwa nchi zaidi ya wiki
mbili zilizopita.
Waandalizi wa maandamano hayo wanaita serikali kuelekeza juhudi zao kwa
wasichana waliopotea .
Mpango ni kuandamana hadi bungeni na kwa mshauri wa taifa wa masuala ya
usalama na kuwasilisha barua ya kutoa wito wa kufanyika kwa juhudi zaidi
kuwanusuru wasichana hao.
Mwanaharakati mmoja wa kijamii amesema katika nchi nyingine yoyote ile suala
la kutekaji nyara wa wasichana hao wengi lingekuwa ni mjadala wa kila siku .
Lakini serikali ya Nigeria imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kukaa
kimwa huku wazazi wenye shauku wakisailia kuwa gizani kuhusu nini
kinachoendelea kuhusiana na wasichana wao.
Huenda kwa kuhisi hilo rais wa Seneti , David Mark, sasa amezungumza.
Amewatolea wito watekaji kuawaachilia mara moja wasichana bila masharti na
akasema bila shaka taifa letu liko vitani .BBC
No comments:
Post a Comment