Baadhi ya wasomi na wachambuzi
wa masuala ya kisiasa hapa nchini wamesema hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadilko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba itasaidia kubadilisha msimamo wa
wajumbe wengi wa Bunge Maalumu la Katiba.
Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba katika Bunge hilo tayari kwa kuijadili, kuiboresha na hatimaye kutoka na Rasimu ya Tatu itakayopigiwa kura ya ama kuikubali kuwa Katiba Mpya au la.
Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba katika Bunge hilo tayari kwa kuijadili, kuiboresha na hatimaye kutoka na Rasimu ya Tatu itakayopigiwa kura ya ama kuikubali kuwa Katiba Mpya au la.
***************************
Majibizano makali yameshuhudiwa
katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo mataifa mengi yameshutumu uamuzi
wa Urusi kunyakua eneo la Crimea,kilele hatahivyo ilikuwa majibizano makali
baina ya mabalozi wa Marekani na Urusi.
****************************
Mazungumzo ya amani kati ya
serikali ya Sudan Kusini na waasi wanaoongozwa na aliyekuwa naibu wa rais wa
nchi hiyo Riek Machar yanatarajiwa kuanza tena leo mjini Addis Ababa Ethiopia.Mazungumzo
hayo yaliahirishwa mapema mwezi huu baada ya mazungumzo ya hapo awali kukwama.
****************************
Mahakama kuu nchini Kenya
imepinga agizo la kutokamatwa kwa mwandishi Walter Baraza baada ya wakili wake
Kibe Mungai kushindwa kufika mahakamani ili kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Hatua hiyo inamaanisha kwamba waziri wa
usalama nchini Kenya Joseph Ole Lenku anaweza kuomba agizo la kukamatwa kwa
mwandishi huyo kabla ya kuwasilishwa katika mahakama ya ICC anakotakikana.
No comments:
Post a Comment