Pages

Thursday, March 30, 2017

NI FURAHA KUWA NA RAFIKI


Ishi na rafiki kwa akili kubwa mpe nafasi sababu katika siku usiyoidhania anaweza kuwa adui mkubwa sana  kwako,Wakati huo huo ishi na adui kwa akili sababu huwezi jua kuna siku anaweza kuwa rafiki yako.

Wednesday, April 13, 2016

HABARI KWA UFUPI




Siku moja baada ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Anne kilango kuvuliwa uongozi kwa kutosema ukweli,Mkuu wa wilaya ya kishapu Hawa Nghubi ameiruka taarifa ya kutokuwepo kwa watumishi hewa ambayo amesema ilimshtua alipoiona kwenye televisheni.

Tuesday, April 12, 2016

LA KWETU CONCERT NI TAMASHA KUBWA NA LA KIHISTORIA LINAKUJA KUTIKISA TANZANIA

Tamasha la LA KWETU CONCERT ni Tamasha kubwa na la kihistoria linakuja kupinga mauaji ya ndugu zetu Albino,na uzinduzi wake utafanyikia Mwanza na hivyo kuweza kuzunguka kanda ya ziwa yote na hatimaye kuzunguka nchi nzima.


Monday, April 20, 2015

HABARI KWA UFUPI




Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitaka jumuiya ya albino nchini kuisukuma Serikali ili Rais Jakaya Kikwete asaini utekelezaji wa hukumu ya kuwanyonga wauaji wa albino.Kauli ya Lowassa imekuja wiki moja tu baada ya Rais Kikwete kusema hajapelekewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya albino kutokana na mlolongo mrefu wa kisheria uliopo kabla ya kumfikia.

Friday, April 17, 2015

HABARI KWA UFUPI




Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilizindua mkakati wake wa ushindi “Hakuna kulala, hakuna kula mpaka kieleweke” katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kwa kufungua mafunzo yatakayoendeshwa nchi nzima kwa viongozi wa vyama na Serikali za Mitaa

Wednesday, April 08, 2015

POLISI MWINGINE AUA MTU MWEUSI MAREKANI

Wakuu katika jimbo la South Carolina nchini Marekani wamemhukumu Afisa mmoja wa polisi mweupe, kwa kosa la mauaji.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumpiga risasi raia mmoja mweusi na kumuuwa.
Picha ya Video ya kilichofanyika imewekwa mtandaoni.

Mkanda huo wa video unaonesha mtu mmoja kwa jina, Walter Scott, akipigwa risasi alipokuwa akimkimbia afisa huyo.BBC

Monday, March 30, 2015